Wednesday, June 13, 2012

TANZANIA FOOTBALL NEWS: MAXIMO KUTUA JUMAPILI


B
aada ya siku chache zilizopita website hii ilikuwa ya kwanza kuripoti kwamba klabu ya Yanga ipo katika hatua za mwisho za kumsaini Marcio Maximo, leo hii imefahamika kwamba kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa 'Taifa Stars' Mbrazil, Marcio Maximo anatarajia kutua nchini kwa mara nyingine tena toka aondoke nchini mwezi juni mwaka 2010 siku ya jumapili juni 17 saa 9 alasiri.

Maximo anakuja nchini kuchukua mikoba ya Mserbia wa Yanga Kostadin Papic aliyenyimwa mkataba mpya, baada ya ule wa awali wa miezi 6 kuisha wakati ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2011/12 ukielekea mwishoni.

Maximo awali alitarajiwa awasili nchini hapo kesho, na kwa mujibu wa taarifa rasmi na zinasema kocha huyo mwenye msimamo mkali atawasili jumapili na shirika la ndege ya Emirates.

No comments:

Post a Comment