Friday, June 29, 2012

BOLT, BLAKE NA POWELL WAKARIBIA KUFUZU OLIMPIKI.

Usain Bolt.

WANARIADHA nyota wa mbio fupi wa Jamaica Usain Bolt, Yohan Blake na Asafa Powell wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya mbio za taifa za kufuzu michuano ya Olimpiki kwa mwaka huu. Bingwa mtetezi wa michuano ya olimpiki Bolt alitumia muda wa sekunde 10.06 akitanguliwa na Blake aliyetumia muda wa sekunde 10.00 wakati Powell alishika nafasi ya tatu kwakutumia muda wa sekunde 10.19. Nusu fainali na fainali ya mbio hizo inatarajiwa kufanyika baadae leo katika Uwanja wa Taifa jijini Kingston ambapo washindi watatu ndio watakaofuzu michuano ya olimpiki ambayo itafanyika jijini London. Bolt anayeshikilia rekodi ya dunia ambaye alishinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 100, 200 na 400katika michuano iliyofanyika Beijing mwaka 2008 ndio anayeshikilia rekodi ya mkimbiaji mwenye kasi kwa mwaka huu baada ya kutumia muda wa sekunde 9.76 katikambio zilizofanyika jijini Rome mwezi uliopita. Mkimbiaji nyota wa Uingereza Dwain Chambers alifanikiwa kufuzu michuano hiyo baada ya kutumia muda wa sekunde 10.25 wakati kwa upande wa Marekani Justin Gatlin na Tyson Gay wote walifanikiwa kufuzu wakitumia muda wa sekunde 9.80 na sekunde 9.86.

No comments:

Post a Comment