Saturday, June 30, 2012

TANZANIA FOOTBALL NEWS: YANGA YAIBAMIZA EXPRESS YA UGANDA 2-1

Mechi kati ya Yanga na Express ya Uganda, Yanga wameshinda magoli 2-1, mabao yote yakitiwa kimiani na Jerry Tegete kipindi cha kwanza. Katika kipindi cha kwanza Yanga ilitawala mchezo kwa asilimia 60 dhidi ya Express hata hivyo katika kipindi cha pili mambo yamebadilika ambapo timu ya Express ya Uganda imefanikiwa kupata goli moja la kufutia machozi na kufanya matokeo kubaki hayohayo 2-1.Kikosi kilichoanza Yanga, kutoka kulia waliosimama Ally Mustafa 'Barthez', Athumani Iddi 'Chuji', Said Bahanuzi, Oscar Joshua, Jerry Tegete na Nizar Khalfan. Walioinama kutoka kulia ni Kelvin Yondan, Nadir Cannavaro, Juma Abdul, Frank Damayo na Simon Msuva. 

No comments:

Post a Comment