Friday, June 29, 2012

MBEYA UPDATE: SOCCER BONANZA YAPEWA BARAKA


M
wenyekiti wa Chama cha Soka wilaya ya Mbeya (MUFA) Selemani Haroub ametoa baraka zake zote kufanyika kwa Bonanza la mchezo wa soka linalojulikana kama “ SOCCER FIESTA BONANZA”.

Haroub amesema Soccer Fiesta Bonanza linaweza kuibua vipaji vya soka katika wilaya ya Mbeya Mjini na Mkoa kwa ujumla.

Hii leo majiraya saa Mbili Kamati ya Maandalizi ya Soccer Bonanza Fiesta inayoongozwa na Shafii Dauda itakabidhi vifaa kwa timu shiriki katika ukumbi wa The VIBE CLUB, uliopo Jijini Mbeya karibu kabisa na Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Bonanza hilo limejikita katika soka kwa klabu kubwa 8 za barani Ulaya zenye mashabiki wa kutosha ambazo ni Real Madrid, Barcelona, Man UTD, Man City, Arsenal, Chelsea, Liverpool na Bayern Munich.

No comments:

Post a Comment