Saturday, June 30, 2012

GLOBAL NEWS: HOLLANDE KUHALALISHA NDOA ZA JINSI MOJA NA WATOTO WA KUPANGA

Rais Mpya wa Ufarana Francois Hollande ameahidi katika kampeni yake kuhalalisha kuwa na mtoto wa kupanga kisheria pamoja na ndoa ya jinsia moja katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
 
Hakuna muda maalumu uliotolewa kwa ajili ya kuanza kutekelezwa kwa sheria hiyo. Kama sheria hiyo itapitishwa, Ufaransa itajiungana na mataifa mengine sita barani Ulaya ambapo ndoa za jinsia moja na kuwa na mtoto wa kupanga kunaruhusiwa. Kwa hivi sasa Ufaransa inaruhusu ndoa ya jinsia moja tu.

No comments:

Post a Comment