Friday, June 29, 2012

WASIFU 360: LADY GAGA

Stefani Joanne Angelina Germanotta[6] (amezaliwa tar. 20 Machi, 1986) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo za pop dansi kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Lady Gaga.Gaga, alizaliwa mjini Yonkers, New York na kukulia mjini Manhattan, ambako alijiunga na shule ya kulipia ya Convent of the Sacred Hearthalafu baadaye akaelekea zake katika Chuo Kikuu cha New York (Tisch School of the Arts).

Akiwa na umri wa miaka 20, alianza kufanya kazi na Interscope Records akiwa kama mtunzi wa nyimbo, akatunga nyimbo kadhaa kwa ajili ya kundi la muziki wa pop la Pussycat Dolls. Gaga, ana athira kubwa kabisa na wanamuziki wa rock kama vile David Bowie na timu nzima ya bendi ya rock maarufu ya Queen na vilevile waimbaji wa muziki wa pop wa miaka ya 1980 kama vile Madonna na Michael Jackson.

Kuiingia kwake kwenye sanaa kumesababishwa na mtunzi wa nyimbo na mtayarishaji wa rekodi za muziki maarufu kama Akon, aliyegundua ya kwamba, Gaga, pia ana kipaji cha sauti, na akaingia naye mkataba wa kurekodi kwenye studio yake ya Kon Live Distribution, na kisha baadaye aanze kufanya kazi zake mwenyewe kwa ajili ya albamu yake ya kwanza.
Mnamo mwaka wa 2008, Gaga ametoa albamu yake ya kwanza iitwayo The Fame, ambamo alielezea kwamba "namna gani mtu anavyoweza kujsikia kwa kuwa maarfu". Leo hii, albamu imetoa vibao vyake vikali kadhaa vilivyomaarufu kama vile "Just Dance" na "Poker Face ", ambayo awali ilipewa Tuzo ya Grammy ikiwa kama wimbo bora wa kudansi - katika ugawaji wa 51 wa Tuzo hizo za Grammy.

Wasifu

Maisha ya awali

Gaga alizaliwa mnamo tar. 20 Machi, 1986mjini Yonkers, New York na baba (ambaye kabaila wa mtandao) na mama (ambaye mfanyabiashara mwenzi wa baba), ambao wote ni Waitalia.[7][8]Akiwa mtoto, alijiunga na Shule ya Kikatoliki ya Convent of the Sacred Heart.[9]Alianza kujifunza piano kwa kusikia tanguu akiwa na umri wa miaka minne, na akaja kuandika noti zake za piano kwa mara ya kwanza akiwa na umiri wa 13 na akaanza kutumbuiza kwenye matamasha madogomadogo akiwa na umri wa miaka 14.
Akiwa na umri wa miaka kumi na saba, Gaga akawa mmoja kati ya watu ishirini wa dunia nzima kupata elimu ya muziki ya chuo kikuu cha New York cha Tisch School of the Arts. Aliboresha akili zake za kuandika kwa njia ya kuandika insha na ripoti kuhusu mada kama sanaa, dini, na siasa na jamii.[10]
Alitoka katika nyumba aliokuwa akiishi na wazazi wake,[11] na kuanza kujirusha mitaani, huku akiwa ana tumbuiza katika klabu za mitaani kwao na kisha baadaye akawa anafanya kazi na bendi ya Mackin Pulsifer na SGBand. Akajikuta akizungukwa na waimbaji kibao ambao wanaimba staili sawa na ile ya muziki wake yeye anaoimba, na ndipo alipoamua kufanya mtindo mkali kabisa kwa kutumia staili ya rock 'n roll huku kwa mbali anatia muziki wa pop.[12]Baba yake alishtushwa na kwa kuona kitendo cha mwanawe kuzurula mitaani na kujibwaga kwenye mabaa huku akionekana anafanya shoo na baadhi ya machangudoa wala unga na wale wacheza uchi kwenye mabaa ya usiku. Gaga alisema:
"Baba hakuweza kunitazama kwa miezi kadhaa"
alikiri kwa jaribio lake la awali. Na kusema: "Nilikuwa kwenye mkia wa mwiba, kwa hiyo ni vigumu kwa yeye — kuelewa yale.
Gaga alipata jina lake la kisanii pale mtayarishaji wa muziki Rob Fusari alipoifananisha staili ya sauti yake na hayati Freddie Mercury na kuchukua jina la 'Gaga' kutoka katika wimbo wa bendi ya Queen wa "Radio Ga-Ga". Fusari ndiyo aliyemsaidia Gaga kutunga vibao vyake vya awali, ambavyo vinajumuisha "Disco Heaven", "Dirty Ice Cream" na "Beautiful, Dirty, Rich".

Muziki

Albamu'

EP

  • 2009: 'The Cherrytree Sessions
  • 2009: The Fame Monster
  • 2009: Hitmixes
  • 2010: The Remix

No comments:

Post a Comment