A |
lpha Blondy(Alizaliwa kama Seydou Koné, tar. 1 Januari, 1953mjini Dimbokoro, Côte d'Ivoire, Afrika ya Magharibi), ni mwanamuziki wa Reggae na msanii anayerekodi nyimbo zake nyingi kimataifa.
Alpha Blondy mara nyingi huimba kwa lugha ya kidioula ambayo ndio lugha yake ya taifa huku akichanganya Kifaransana Kiingereza, Lakini pia wakati mwingine huimba kwa Kiarabu au Kiyahudi. Mashairi yake yanamanisha siasa kali yenye mwelekeo na uchangamfu.
Maisha ya Mwanzo
Alpha ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto tisa, Jina la kuzaliwa ni Seydou Kone amezaliwa mjini Dimbokro mnamo 1953. Alilelewa na bibi yake mzaa mama. Mnamo mwaka 1962, Alpha Blondy alikwenda kukaa na baba yake aliyekuwa anaishi mjini Odienne, Ambapo alikaa kwa muda wa miaka kumi, Baadae akijiunga na shule ya Sainte Elisabeth high school, na kujishughulisha na makundi ya wanafunzi ya Ivory Coast. Hapo ndipo alipo unda bendi. Ingawaje, Upenzi huu uliathiri masomo yake na baadae Blondy alikufukuzwa shule kutokana na maudhulio mabovu shuleni.
Wazazi wake Alpha wakampleka mtoto wao aAplha kusomea lugha ya Kiingereza mjini Monrovia, mji mkuu wa nchi jirani ya Liberia mnamo mwaka 1973. Huko Alikaa kwa muda wa mwaka mmoja na mwezi mmoja kisha akamia nchini Marekani kwa kuongozea taaluma yake zaidi.
Alivyokuwa Marekani
Mnamo mwaka 1973 Alpha amehamia mjini New York(Pia alishi kidoogo Texas), ni mahali alipomalizia chuo na aliegemea sana kwenye Kiingereza, Kwasabu toka mwanzo alikuwa anataka kuwa mwalimu wa lugha ya Kiingereza.
Alifanya kazi kwa juhudi zote,wakati mwingine hadi usiku, akitafuta hadi kuna kipindi anakuwa mgonjwa. Akiwa New York alikutana na Marastafari kwa mara ya kwanza, Pia alikuwa na uwezo wa kuangalia matamasha ya wanamuziki wa kijamaicakama kina Burning Spear n.k. Wakati huo yeye alikuwa akirekodi nyimbo za kikristo lakini hakuthubutu kuacha kuandika nyimbo zake mwenyewe.
Kwa bahti alikuwa akidodosa sehemu mabalimbali za mjini New York na baade kurudi kidoogo nichi Ivory Coast, Ambako alipata matatizo saana mpaka alivyokuja kukutana rafiki yake waliokuwa wote toka utoto, Fulgence Kassi, Ambaye baadae alikujua kuwa mtayarishaji maarufu wa vipindi vya television. Hapo ndipo alipoanza kuonekana kama kazi yake kweli ni uimbaji, na kutumia jina la 'Alpha Blondy'.
Nyimbo Maarufu
- Jah Glory - Hii aliimba juu ya upigaji vita umaskini.
- Apartheid is Nazism
- Brigadier Sabare - Nyimbo ilihusu ukatili wa maaskari.
- Cocody Rock - Hii ilikuja kuwa ndio kama nyimbo yake ya taifa kila mtu anajua kuimba.
- Guerre Civile - Hii ilihusu masuala ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.
- Jerusalem- Hii ilataka amani nchini israel. Nyimbo inaanza na maneno yanatumiwa katika sara za kiyahudi, Hivyo aliaza kiyahudi.
- Journalistes en danger - Hii ilihusu mauaji ya Norbert Zongo aliyekuwa mchapishaji na mhriri wa gazeti la Independent la nchini Burkina Faso.
- Politiqui - Hii ilihusu uraia.
- Yitzhak Rabin
Albamu alizotoa
- 1982: Jah Glory
- 1984: Cocody Rock!!!
- 1985: Apartheid Is Nazism
- 1986: Jerusalem (Alpha Blondy album)|Jerusalem (Akiwa na Wailers Band|The Wailers)
- 1987: Revolution (Alpha Blondy album)|Revolution
- 1989: The Prophets (album)|The Prophets
- 1992: Masada (album)|Masada
- 1993: SOS Guerres Tribales
- 1993: Live Au Zénith (Paris)
- 1994: Dieu
- 1996: Grand Bassam Zion Rock
- 1997: Best Of (Alpha Blondy album)|Best Of
- 1998: Yitzhak Rabin (album)|Yitzhak Rabin
- 1999: Elohim (Alpha Blondy album)|Elohim
- 2001: Blondy Live Paris Bercy
- 2002: Merci
- 2005: "Akwaba"
No comments:
Post a Comment