Thursday, June 28, 2012

TANZANIA ECONOMIC NEWS: TANESCO YAJA NA NEEMA KWA WATEJA

S
HIRIKA la Umeme Tanzania(Tanesco), limesema ifikapo leo litakuwa limeshawaunganishia umeme wateja wake wote walioomba kupata huduma hiyo kwa muda mrefu.

Hayo yamesemewa jana na meneja uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Amesema kwa sasa shirika hilo lina vifaa vya kutosha na kwamba ndicho kitu ambacho kilikuwa kikiwakwamisha kutekeleza majukumu yao.

Amesema wateja ambao walikuwa wameomba wafike katika ofisi za Tanesco katika maeneo yote zilizopo ofisi zao ili waweze kupatiwa huduma hiyo.

Amesema hakuna mfanyakazi wa Tanesco anayepaswa kumzungusha mteja wa shirika hilo hivyo mteja yeyote atakayezungushwa awasiliane na makao makuu ili waweze kushughulikiwa.

Katika hatua nyingine Tanesco imesema  wanatarajia kuzindua mtambo wao mpya wa megawati 100 unaoiwa Jacobsen.

Badra amesema mtambo huo utazinduliwa kesho na kwamba ongezeko la megawati hizo 100 utafanya nchi iwe na megawati 800 za umeme.

No comments:

Post a Comment