Saturday, June 30, 2012

AFRICA NEWS: MURSI ALA KIAPO

Rais mteule wa Misri, Dk. Mohammad Morsi jana amekula kiapo cha urais mbele ya Mahakama Kuu ya Katiba ya nchi hiyo.

Katika sherehe hizo Muhammad Mursi ameapa kwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba, atalilinda taifa, kuheshimu katiba, sheria za nchi yake sambamba na kulinda maslahi ya taifa la Misri. Amesema kuwa, leo taifa la Misri linashuhudia maisha mapya na kwamba uhuru na demokrasia vinaanza kufanya kazi.
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Misri Faruq Sultan amemtakia rais huyo mteule mafanikio katika harakati za kulijenga taifa hilo. Hapo jana Mursi alikula kiapo mbele ya makumi ya maelfu ya watu katika Medani ya Tahrir hatua ambayo awali ilipingwa vikali na Baraza la Kijeshi la nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment