Thursday, June 28, 2012

GLOBAL NEWS: UTURUKI HAITAIVAMIA SYRIA

W
aziri Mkuu wa Uturuki ametangaza kuwa Ankara haina mpango wowote wala nia ya kuishambulia Syria baada ya nchi hiyo kuitungua ndege yake ya kijeshi.

Rajab Tayyeb Erdogan Waziri Mkuu wa Uturuki amedai kuwa Ankara imezingatia hatua zote katika kukabiliana na kitisho chochote kinachoweza kutokea dhidi ya umoja wa ardhi ya Uturuki lakini nchi hiyo kamwe haiwezi kuwa na mtazamo wa kiadui dhidi ya ardhi za nchi nyingine.
Waziri Mkuu wa Uturuki alidai juzi akilihutubia bunge la nchi hiyo kuwa serikali ya Rais Bashar al Assad wa Syria ni hatari kubwa kwa usalama wa Uturuki. Erdogan aliongeza kuwa hatua ya Syria ya kuitungua ndege ya Uturuki haitaachiwa bila ya jibu.

No comments:

Post a Comment