Thursday, June 28, 2012

TANZANIA BOXING NEWS: TPBC YATAMBUA MKATABA WA CHEKA NA SIYAJI


K
amisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) inatambua mkataba (mikataba) kati ya Francis Cheka na Kaike Siyaji aliyosaini kupigana na Japhet Kasheba siku ya July 7, mwaka huu.

Aidha Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) inamshauri bondia Francsi Cheka awe na mawasiliano mazuri na promota wa pambano hilo ili hali ya kutoelewana iliyokwisha kujitokeza imelizwe kwa manufaa ya tasnia ya ngumi nchini.

TPBC inawashauri wadau wote wanaotaka kufikia makubaliano na mabondia kutofanya hivyo nje ya utaratibu wa mchezo wa ngumi ambao ni kusaini mikataba mbele ya Kamisheni na wakili ili maslahi ya wote yalindwe.

Tunapenda pia kuwashauri mabondia wote kuacha tabia ya kusaini mikataba zaidi ya mmoja hususan wakati bado wakiwa na pambano mkononi.

Imetolewa na,
Onesmo A.M.Ngowi
President, Tanzania Professional Boxing Commission(TPBC)
Benjamin William Mkapa Pension Towers
Mezzanine Floor, Azikiwe Street
Dar-Es-Salaam - Tanzania
Technology House, 35-38 Ghalla Road,
P.O BOX 1106, Moshi - Tanzania

No comments:

Post a Comment