Friday, June 29, 2012

TANZANIA SOCIAL NEWS: IDD AZZANKUWA MGENI MAHAFALI LEO KINONDONI MUSLIM


MBUNGE wa Kinondoni, Bw. Idd Azzan atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za wanafunzi waliomaliza shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim (Reunion) zitakazofanyika leo Jumamosi Juni 30.

Mwenyekiti wa Reunion Bi. Mambo Tambaza alisema katika sherehe hizo ambazo zitahudhuriwa na wanafunzi waliowahi kusoma shule hiyo kutoka ianzishwe mwaka 1966, walimu waliowahi kufundisha shule hiyo na wanafunzi wanasoma watahudhuria.

Makamu Mwenyekiti wa Reunion, Bw. Aboubakar Liongo amesema maandalizi ya sherehe hiyo yamekamilika na sherehe hiyo itaanza saa 5 asubuhi kwenye hoteli ya Cine Club iliyopo Kawe, Dar es Salaam.

Ametoa wito kwa wanafunzi waliowahi kusoma shule hiyo kujitokeza ili kufahamiana na kuangalia uwezekano wa kuisaidia shule hiyo.

"Tumetoa taarifa kwa wanafunzi wote kwa njia ya mtandao na ujumbe mfupi wa simu za mkononi, ni matumaini yetu kuwa wengi watahudhuria" alisema Bw. Liongo.

Katika sherehe hizo mkuu wa shule hiyo na wanafunzi wanaosoma wataeleza hali ya kitaaluma katika shule hiyo na msaada wanaohitaji.

No comments:

Post a Comment