Friday, June 29, 2012

MBEYA UPDATE: UJUMBE WA SERENGETI FIESTA BONANZA WAWASILI

U
jumbe wa Serengeti Fiesta Bonanza umewasili jioni ya jana Jijini Mbeya kwa madhumuni ya kuendeleza harakati zake za kutafuta vipaji mkoani Mbeya katika tasnia ya muziki.
 SHAFII DAUDA AKISHUKA KWENYE BASI WAKATI WALIPOWASILI KATIKA KITUO CHA REDIO MBEYA FM
 
Ujumbe huo ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Maandalizi ya Serengeti Fiesta Super Nyota Sebastian Maganga umewasili majira ya saa 2 usiku na kupokelewa na Redio Mbeya FM.

Madhumuni makubwa ya kufika katika Kituo cha Redio Mbeya FM yalikuwa kufanya mahojiano maalum kuhusu siku ya leo ya Jumamosi katika Serengeti Fiesta Super Nyota na Kesho Jumapili katika Soccer Fiesta Bonanza .

Mratibu wa Soccer Fiesta Bonanza Shafii Dauda alizungumza masuala kadha wa kadha kuhusu Soccer Fiesta Bonanza itakayofanyika katika viwanja vya TIA jijini hapa na kuongeza kuwa kiingilio ni jezi ya timu  husika inayoshabikiwa kama hakuna basi kiingilio ni shilingi 1,000/=.

Soccer Fiesta Bonanza inashirikisha mashabiki wa timu 8 barani Ulaya ngazi ya klabu ambao ni EL Classico, Man UTD, Man City, Arsenal, Chelsea na Liverpool ambazo mkoani Mbeya zimeonekana kuwa na mashabiki wengi.

Katika Usiku wa Mashabiki ndani The VIBE Club kulishuhudiwa watu wakiwa na sahauku kubwa ya kushuhudia tamasha hilo la Jumapili huku kukitokea vuta ni kuvute nani atayeibuka mshindi.

Shafii Dauda ameongozana na kina Alex Luambano, Mbwiga Mbwiguke  na wengine akali ya 5 kwa ajili ya kufanikisha show hiyo.

EURO VIBE FANS ZONE
Taarifa kutoka The VIBE Club zinasema kesho Jumapili  mara baada ya kumalizika kwa Soccer Fiesta Bonanza  katika viwanja vya TIA kutakuwa na Euro Vibe Fans Zone katika Vibe Outdoor ambako mashabiki wa Soka watakutana tena kutaza fainali ya michuano ya UEFA Euro 2012 baina ya Hispania na Italia kutafuta mshindi wa michuano hiyo mwaka huu.

No comments:

Post a Comment