Friday, June 29, 2012

FREEMASONRY AND JABIR JOHNSON:SEHEMU YA 16: TAFSIRI KATIKA UISLAMU

LEO KATIKA UMASONI tutajikita hasa na Mawazo ya Mwenyekiti: ‘Abdullaah Bin Humayd. Makamu Mwenyekiti: Muhammad bin ‘Aliy al-Harkaan.  Wajumbe: ‘Abdul ‘Aziyz bin ‘Abdullaah bin Baaz (Allaah Amrehemu) na Muhammad Mahmuud as-Sawaaf.

Imefasiriwa na: ‘Abdun-Naaswir Hikmany



Umasoni ni chama cha siri kabisa cha Kiyahudi, kimeanzishwa huko enzi za Kiroma sehemu za Aurshalim (Jerusalem) wakati wa ufalme wa Herodus Aghriba baina ya mwaka 37-44 M, aliyekuwa mjukuu wa Herodus Mkuu, muuaji wa watoto wa Bethlehem kwa khofu ya kutokea Yesu, ambaye kwa mujibu wa imani zake, aliazimia kuondosha haraka iwezekanavyo utawala wote wa Herodus.

Umasoni ulitambulika kwa utata wake na mtindo wake ulio na amri madhubuti. Malengo yake ni kuhakikisha mamlaka yanabaki kwa Mayahudi duniani kote. Unahubiri upagani, utenganifu wa jamii na upotofu. Jumuiya hii inachagua wajumbe wake miongoni mwa watu maarufu kwenye nyanja ambazo zina nafasi kisiasa, kiuchumi au kijamii. Kitabu cha Simplified Encyclopedia kimeandika na kuchapisha kutoka WAMY (Baraza La Vijana Waislamu Duniani - World Assembly of Muslim Youth – Saudi Arabia) kinafafanua kwamba muasisi wa jumuiya hii ni Herdous Aghriba (44 M) mfalme wa Kiroma kwa msaada wa wasaidizi wa Kiyahudi.

Hivyo, mwanzo wake ulitokana na ujanja, hila na mageuzi. Inachagua zana za utambulisho, majina na alama ili kueneza khofu na kuwafanya watu kuamini katika habari zisizo sahihi. Rabai Laquiz amesema: “Umasoni ni ya Kiyahudi kwa mujibu wa historia yake, uongozi wake, mafundisho yake, zana zake za siri na kazi zake za ubunifu wa hali ya juu... Ni ya Kiyahudi kuanzia utosini hadi miguuni. Ilikuwa ikiitwa: ‘Uwezo wa siri wenye lengo la kuwaadhibu Wakristo, kuwauwa viongozi, kuwakata vichwa, kuwapiga pande na kuizuia dini yao kuenea.’ Sasa, imechukua jina hili (Umasoni – Freemasonry) kwa kipindi cha karne kadhaa”.

Neno “mason” lina maana ya yule mwenye kujenga nyumba. Hivyo “Free masons” lina maana ya Wamasoni walio huru. Hii ndio ilikuwa haswa alama yao wakati walipokuwa wakifanya kazi zao (za kujenga nyumba). Lakini sasa jina hilo lipo mbali na tafsiri hii. Enzi hizo ndio zilikuwa mwanzo wa umoja huu. Lakini vitu vilianzia tokea 177 M pale Adam Webshawit, Mkristo aliyeingia kwenye upagani, alipovutiwa na umoja huu ambao alidhani utamsaidia kuimiliki dunia yote.

Mara ya mwisho kutimu kazi hii ilikuwa ni mwaka 1776 M, na bodi ya mwanzo kuanzishwa ndani ya kipindi hicho (Bodi ya Torani) ilipewa jina baada ya huyo Shetani wao waliokuwa wakimwabudia. Ukweli ni kwamba, Webshawit alikuwa ni mtu wa mwanzo aliyeanzisha mipango ile ile ya Umasoni.


Azma ya mwanzo ya Umasoni ni kuupiga vita “Ukristo”. Baadaye, azma zao ziliendelea kupiga vita dini zote, kuirudisha tena Israel na kuitoa Palestine.


No comments:

Post a Comment