Tuesday, June 12, 2012

NASRI AFAFANUA USHANGILIAJI WAKE.

KIUNGO wa kimataifa wa Ufaransa, Samir Nasri amebainisha kuwa tukio lake la kushangilia kwa hasira baada ya kusawazisha bao katika mchezo wa kundi D michuano ya Ulaya baina ya timu yake na Uingereza ambapo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, alikuwa amemlenga mwandishi wa jarida moja nchini kwake la L’Equipe. Mchezaji huyo ambaye pia anakipiga katika klabu ya Manchester City alikuwa akikimbia kuzunguka uwanja mara baada ya kusawazisha bao hilo dakika ya 39 huku akiwa ameweka kidole chake kwenye mdomo akimaanisha watu waache kuongea na kunyamaza. Ushangiliaji huo ulizua mijadala katika mtandao wa kijamii wa twitter ambapo baadhi watu walidai kuwa mchezaji huyo alifanya hivyo kuvilenga vyomba vya habari vya Uingereza pamoja na benchi la ufundi la timu pinzani. Hatahivyo Nasri alifafanua tukio lake hilo kuwa alimlenga mwandishi wa habari wa L’Equipe ambaye alikosoa kuhusu kuitwa kwake katika kikosi cha timu hiyo akidai hana kiwango. Nasri amesema kauli ya mwandishi huyo ilimkasirisha mama yake ambaye ni mgonjwa kwa mizei kadha sasa.

No comments:

Post a Comment