Tuesday, June 12, 2012

EURO 2012: UEFA YAOMBA ULINZI ZAIDI KUDHIBITI UBAGUZI.

SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limezitaka miji ya nchi wenyeji wa michuano ya Kombe la Ulaya, Poland na Ukraine kupeleka polisi katika viwanja ambavyo timu zinazoshiriki michuano hiyo zinafanya mazoezi ili kudhibiti suala la ubaguzi wa rangi. Ombi hilo ambalo pia linataka polisi kuwafungulia mashtaka watakaofanya makosa hayo, limekuja kufuatia baadhi ya mashabiki kushangilia kama nyani wakiwalenga baadhi wachezaji weusi wa timu ya Uholanzi katika mazoezi yao jijini Krakow, Poland. Katika taarifa yake UEFA wamesema tayari wamemtumia barua Waziri wa Michezo wa Poland pamoja na mameya wa miji wenyeji wa michuano hiyo kufuatilia suala hilo kwa karibu ikiwemo kuongeza ulinzi wa polisi wakati wa mazoezi ya timu zinazoshiriki. Shirikisho hilo pia limeagiza kuwa mtu yoyote atakayepatikana na makosa hayo anatakiwa kuondolewa uwanjani mara moja na kufunguliwa mashitaka ya kosa la jinai ili kudhibiti vitendo hivyo ambavyo havikubaliki michezoni.

No comments:

Post a Comment