Sunday, June 24, 2012

MBEYA UPDATE: WANAKIJIJI WA ISUNURA WAKATAA KUCHAGUA MABALOZI


W
ANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kijiji cha Isunura wilayani Mbarali Mkoani Mbeya, wamekataa kufanya uchaguzi wa Mabalozi wa chama hicho kwa madai kuwa viongozi wao ngazi ya wilaya ya Serikali ya wilaya hiyo kushindwa kuwaunga mkono wananchi wa kijiji hicho kuwajibika katika kata Mawindi.

Wakizungumza na waandishi wa habari waliofika kijijini hapo, wamesema kuwa mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu kutokana na maslahi ya kiutawala kwa viongozi wa Serikali na chama hicho kwa  kuendelea kuwalazimisha wananchi wa kijiji hicho kutaka kuwapeleka katika kata Mpya ya Igava ambapo wananchi hawaitaki wakitaka kuendelea kuwajibika katika kata yao ya zamani ya Mawindi.

Wamesema kuwa wao hawakufanya uchaguzi huo wa mabalozi uliofanyika mwezi mei mwaka huu nchini kote kwa madai kuwa viongozi wa chama hicho pia wamaeonekana kuwa na usaliti kwa wanachama wake ambapo umekuwa ukiwageuka kila wanapo kwenda kutoa malamaliko yao kwa vielelezo.

Wamesema hawataki kuwajibika katika kata ya Igava kutokana na ramani na miundombinu iliyopo lakini Serikali imekuwa ikiwalazimisha kwa muda mrefu sasa.

Mwenyekiti wa tawi la Isunura Chesco Mduba alisema kilichowapelekea kukataa kufanya uchaguzi wa mabalozi kijijini hapo ni kutokana na viongozi wa serikali na wa CCM kuwapuuza wananchi kuhusu mpaka huo huku wakiendelea kuwalazimisha.

Amebainisha kuwa mgogoro huo ulianza mwaka 2010 baada ya kata ya Mawindi kugawanywa na kupatikana kata tatu ambazo ni kata ya Igava, Ipwani na Mawindi yenyewe huku kukiwa na vijiji vitano kila kata. Amesema kufuatia hali hiyo kijiji cha Isunura kinapaswa kuwa kata ya Mawindi ili kukamilisha vijiji vitano lakini kutokana na baadhi ya watu kutoka kijiji cha Isunura kutaka madaraka ya uongozi wanataka kulazimisha kukipeleka kijiji hicho kata ya Igava ambyo kwa sasa ina vijiji vitano huku kata ya Mawindi ikiwa na vijiji vinne.

Mbali na kukataa kufanya uchaguzi wa mabalozi katika kijiji hicho ambacho kingekuwa na jumla ya mabalozi 25, viongozi wa chama hicho na wafuasi wake walisema kuwa wanaandaa utaratibu wa kwenda ofisi ya Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya kueleza yanayowasibu.

Hata hivyo imebainika kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Nawaab Mulla anatokea wilayani Mbarali lakini hajui mambo mengi yanayokikabili chama chake wilayani humo na hata baadhi ya wilaya anazoziongoza kwa sasa hali inayomwakikishia kutoweza kutetea nafasi yake katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Mwezi Agosti Mwaka huu.

No comments:

Post a Comment