V |

Mratibu wa maonyesho hayo Peter Oguwi amesema maonyesho hayo yatakayoanza julai 10 hadi 14 yatafanyika katika viwanja vya nane nane njiro.
Pia yatashirikisha vyuo kutoka nje ya afrika mashariki ikiwemo India maonyesho ambayo ameyaelezea kuwa ni ya kipekee na mara ya kwanza kufanyika na yanatarajia kuleta watu zaidi ya 500.
Oguwi amesema lengo la maonyesho hayo ni kutangaza huduma zinazotolewa na vyuo hivyo zikiwemo program mbalimbali ilikuwafanya wananchi wanchi hizo kuthamini vyuo vyao badala ya kukimbilia nchi za nje hivyo maonyesho hayo yana tarajia kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu ya juu.
Waziri wa elimu na ufundi Shukuru kawambwa anatarajiwa kufungua rasmi maonyesho hayo July 11 mwaka huu Jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment