Tuesday, June 12, 2012

GLOBAL NEWS: WAZIRI WA PILI KUWAIT AJIUZULU


W
aziri wa masuala ya jamii na kazi nchini Kuwait amejiuzulu. Waziri huyo, Ahmed al-Rujaib, ni wa pili kujiuzulu katika muda wa majuma kadhaa baada ya kushinikizwa na wabunge wa upinzani.
Wachambuzi wanaamini hatua hiyo huenda ikasababisha mabadiliko kamili ya baraza la mawaziri au kujiuzulu kabisa kwa serikali ya sasa ilioundwa baada ya uchaguzi wa mapema mwezi februari. Hiyo ni serikali ya nne katika  muda wa miaka sita. Wabunge wa upinzani wamekuwa wakidai wapewe nafasi ya kumhoji waziri  al-Rujaib bungeni  wiki ijayo, wakitaka ajibu maswali kadhaa ikiwa ni pamoja  na kuongezeka kwa bei ya  bidhaa muhimu, udhibiti wa ubora wa chakula, vibali vya ukaazi na makampuni haramu.

No comments:

Post a Comment