Tuesday, June 12, 2012

LEO KATIKA HISTORIA: MIALE YA JUA YAKUSANYWA


12 Juni 1914, 
Kwa mara ya kwanza kabisa yalifanyika majaribio ya kutumia nishati ya joto la jua pambizoni mwa Cairo mji mkuu wa Misri. Mbunifu na mtekelezaji wa jaribio hilo, alikuwa mwanafizikia mmoja wa Kijerumani, ambaye aliweza kukusanya miale ya jua, na kufanikiwa kuwasha mashine ya mvuke yenye kutumia ' horse power' 50.

No comments:

Post a Comment