Wednesday, June 13, 2012

CASSANO AOMBA RADHI KWA KAULI YAKE.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Italia, Antonio Cassano ameomba radhi kwa kauli yake aliyoitoa kuhusiana na suala la kupinga ushoga. Kauli aliitoa wakati akihojiwa na waandishi wa habari katika michuano ya Kombe la Ulaya ambao walikuwa wakitaka kujua kama baadhi ya wachezaji ambao ni mashoga wapo katika kikosi hicho. Akijibu swali hilo Cassano amesema kuwa kama kweli kuna wachezaji ambao ni mashoga wako katika kikosi hicho basi hilo ni tatizo lao lakini ana matumaini hakuna wachezaji wa aina hiyo katika timu hiyo. Mara baada ya kauli yake hiyo alipata upinzani mkali kutoka katika makundi ya mashoga wakidai ni kauli ya kudhalilisha kitendo ambacho Cassano ilibidi aombe radhi kama kauli yake hiyo iliwaudhi wengine kwani hakukusudia iwe hivyo.

No comments:

Post a Comment