Wednesday, June 13, 2012

VURUGU KUBWA ZATOKEA JIJINI WARSAW.

VURUGU zilizosababishwa na baadhi ya mashabiki wa Poland na Urusi kabla na baada ya mchezo baina timu hizo uliochezwa jana zimesababisha watu 15 kujeruhiwa na wengine zaidi ya 100 kuwekwa kizuizini. Baada ya vurugu zilizokuwa zimetawanyika jijini Warsaw kabla ya mchezo huo polisi walilazimika kutumia risasi za mpira kwa baadhi ya makundi ya mashabiki ambao walikuwa wakiwashambulia kwa chupa na mawe karibu na mahali ambapo mashabiki wapatao 75,000 walikuwa wakitizama mchezo huo katika luninga kubwa iliyowekwa eneo hilo. Katika majeruhi hao akiwemo askari polisi mmoja hakuna ambaye yuko katika hatari ya kupoteza maisha, lakini polisi wa eneo hilo wanajaribu kufuatilia picha za video kuangalia uwezekano kama wanaweza kuwagundua watu waliohusika na tukio hilo. Kufuatia tukio hilo mtandao wa mmoja jijini Moscow umetoa taarifa kuwa serikali ya Urusi inamtuma kiongozi wa baraza la haki za binadamu, Mikhail Fedotov kwenda jijini Warsaw kusaidia kushughulikia tatizo hilo lililojitokeza. Baadhi ya mashabiki wapatao 5,000 walikuwa wakitembea kuelekea katika uwanja wa taifa kusheherekea siku ya mapumziko ya kitaifa ya Urusi ambapo kutokana na historia ngumu kati ya nchi hizo mbili ikiwemo Moscow kuitawala Poland wakati wa vita baridi, wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema kuwa mamlaka zinazohusika zisingewaruhusu mashabiki wa Urusi kufanya maandamano.

No comments:

Post a Comment