Sunday, July 1, 2012

MISRI YASHINDWA KUFUZU AFCON KWA MARA YA PILI MFULULIZO.MABINGWA kihistoria Misri wameshindwa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika baada ya kutoa sare ya bao 1-1 dhidi Afrika ya Kati-CAR hivyo kuondolewa kwa jumla ya mabao 4-3 katika michezo miwili waliyocheza. Misri wanaikosa michuano hiyo kwa mara ya pili mfululizo chini ya kocha Bob Bradley ambaye alipewa kibarua cha kukinoa kikosi hicho mwaka uliopita baada ya kushindwa kufuzu michuano ya mwaka 2012. Katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo Misri ilijikuta ikifungwa katika uwanja wa nyumbani jijini Alexandria kwa mabao 3-2 na kuacha mshangao mkubwa miongoni mwa mashabiki wa timu hiyo. CAR imeingia katika mchujo ambao utajumuisha timu 30 ambazo zitacheza hatua ya mtoano ili kupata timu 15 ambazo ndio zitakazofuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika mapema mwakani wakiungana na mwenyeji wa michuano hiyo Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment