Tuesday, July 3, 2012

FREEMASONRY AND JABIR JOHNSON: SEHEMU YA 18,TAFSIRI YA Abdullah Bin Humayd KUHUSU UMASONI

LEO KATIKA UMASONI tutajikita hasa na Mawazo ya Mwenyekiti: ‘Abdullaah Bin Humayd. Makamu Mwenyekiti: Muhammad bin ‘Aliy al-Harkaan.  Wajumbe: ‘Abdul ‘Aziyz bin ‘Abdullaah bin Baaz (Allaah Amrehemu) na Muhammad Mahmuud as-Sawaaf.


Imefasiriwa na: ‘Abdun-Naaswir Hikmany
SEHEMU YA 18
Baadaye, vituo vipya na vingi zaidi vilifunguliwa ndani ya Marekani. Waislamu wengi mno walidanganyika na kauli mbiu ya Umasoni, kisha wakaungana nayo. Lakini, walipotambua malengo yake sahihi, walinawa mikono yao na kuondokana nayo. Wengi wa walioachana na amri hiyo, walikataa kuweka wazi siri zake wakikhofia kuuawa. 

Utafiti mwingi uliofanywa na waandishi wa Magharibi na magazeti ya Kiyahudi pamoja na chunguzi za nyanja makhsusi, zilidhihirisha kwamba Wayahudi wamekuwa wakipanga kuuharibu ulimwengu kupitia “wito wa kutia shime ulio imara” ambao Waislamu ni lazima wauelewe. Kauli mbiu yao maarufu inasema: ‘Dini zinatusababisha kugawana wakati Umasoni inatupeleka kwenye umoja’. Imesimuliwa ndani ya Kitabu cha Masonic Encyclopedia kilichotolewa Phila mwaka 1906 M kwamba kila kituo cha Kimasoni kiwe na nembo ya kudhihirisha sinagogi la Kiyahudi, (na ukweli ni kwamba) kila mwalimu lazima awe mwakilishi wa mfalme wa Kiyahudi na kila mtu wa Umasoni amuajiri mfanyakazi wa Kiyahudi.
 
Ifuatayo ni nukuu kutoka gazeti la Masonic lililotolewa huko London mwaka 1935 M: ‘Shabaha yetu ni kuunganisha amri ambayo wanachama wake watatekeleza mahusiano ya kingono’. Hivyo, walianzisha maeneo (clubs) ambayo watu walitembea utupu na walifanya kila waliwezalo kuharibu thamani ya maadili.

Ili kutimiza malengo yao hapo juu, Wamasoni walianza kutumia majina tofauti kama vile Wana Wa Agano – Children Of Covenant, Kiwanis, Lioness, Yahweh Presence, Exchange, Rotary clubs na nyenginezo.

No comments:

Post a Comment