Tuesday, July 3, 2012

MBEYA UPDATE: WAHABESHI 2 WAKAMATWA

Watu wawili raia wa Ethiopia wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya kufuatia kuingia nchini bila kibali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Maafisa wa Polisi imesema Wahabeshi hao wamekamatwa Julai Mosi mwaka huu katika Kijiji cha Njisi wilayani Kyela majira ya saa 11:40 jioni.

Taarifa hiyo imewataja kuwa ni Solomoni Salepo (23) na Yagala Ababa (20) ambao walikamatwa kufuatia doria ya askari wa Jeshi hilo ambapo walijificha katika nyumba ya Mtanzania Josephat Mwakyando  ambayo Mnyakyusa Jeremiah Leonard (29) alikuwa akiishi.

Maafisa wa Polisi wamesema Jeremeiah Leonard anashikiliwa katika Kituo cha Kasaumulu na anatarajiwa kufikishwa mahakamani

Diwani Athumani Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Jeshi La Polisi mkoa wa Mbeya amewataka wananchi wa maeneo husika kutoa taarifa pindi wanapowabaini wahamiaji haramu.

No comments:

Post a Comment