FIFA. |
TANZANIA imezidi kukwea katika viwango vya ubora vya soka dunia ambavyo hutolewa na Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA kwa kushika nafasi ya 127 ikiwa imepanda kwa nafasi 12 kwenye viwango hivyo. Mwezi uliopita Tanzania ilichupa kutoka nafasi ya 145 mpaka 139 kabla ya mwezi huu kupanda tena na kuzikaribia nchi majirani za Kenya ambayo inashika nafasi ya 125 na Rwanda inayoshika nafasi kama hiyo zote zikiwa zimeporomoka kutoka nafasi walizokuwepo mwezi uliopita. Kenya imeporomoka nafasi 14 kutoka nafasi ya 111 walioyokuwepo mwezi uliopita huku Rwanda wao wakiporomoka nafasi sita kutoka nafasi ya 119 walioyokuwepo msimu uliopita wakati Uganda ndio wanaoongoza kwa nchi za Afrika Mashariki wakiwa katika nafasi ya 85 katika viwango hivyo. Kwa upande wa nchi tano ambazo zinakatia nafasi za juu Hispania wameendelea kuongoza katika orodha hizo wakifuatiwa na Ujerumani ambao wamepanda kwa nafasi moja huku Uruguay ambao mwezi uliopita walikuwa wa pili wakishuka kwa nafasi moja. Uingereza wamepanda kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya sita waliyokuwepo msimu uliopita wakifuatiwa na Ureno ambao wamepanda kwa nafasi tano kutoka ya 10 waliyokuwepo msimu uliopita wakiwa wamechukua nafasi ya Brazil ambayo kwa mara ya kwanza imeporomoka mpaka nafasi ya 11 kutoka ya tano waliyokuwepo mwezi ulipopita.
No comments:
Post a Comment