Pepe Kallé (Novemba 30, 1951 - 28 Novemba, 1998) alikuwa mwimbaji wa soukous, mwanamuziki na kiongozi wa bendi kutoka nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Pepe Kallé alipozaliwa alipewa jina Kabasele Yampanya katika mji mkuu wa Kinshasa(wakati huo mji huu ulikuwa unajulikana kama Léopoldville), lakini baadaye aliamua kulichukua jina la mshauri wake, Grand Pepe Kalle.
Pepe Kalle alikuwa na uwezo wa kuimba kwa sauti ya juu zaidi pamoja na sauti ya chini zaidi ambayo kwa lugha ya kimombo inaitwa “multi-Octave range”. Pepe Kalle alikuwa akiingia jukwani anatambulika mara moja kwani alikuwa na urefu wa sentimita 190 (fiti 6 inchi 3) na uzito wa kilogramu 136 (puandi 300). Mwimbaji huyu alirekodi zaidi ya nyimbo mia tatu na Albamu ishirini katika wasifu wake wa miongo miwili mirefu ya muziki. Kwa wapenzi wake wa muziki alikuwa anajulikana kama "tembo wa muziki Halisi ya Afrika " na "La Bombe Atomique" kwani Pepe Kalle aliwatumbuiza watazamaji tendaji zake za nguvu.

Katika mwaka wao wa kumi tangu kuanzishwa kwao mwaka wa 1982, bendi hii iliteuliwa kama kundi cha juu zaidi nchini Zaire. Katika miaka ya mapema ya 1980, Empire Bakuba iliendelea ziara zake za mbali huku ikitoa zaidi ya albamu nne kwa mwaka. Katikati ya miaka za 1980, walikuwa na wafuasi wengi katika Kati ya Francophone na Afrika Magharibi. Ushirikiano wake wa mwaka wa 1986 pamoja na Nyboma iliyokuwa ikiitwa Zouke Zouke ilikuwa mmoja kati ya Albamu zilizouzwa sana mwaka huo. Lakini ilikuwa ushirikiano wake wa pili na Nyboma, Moyibi (mwaka wa 1988), ambayo ilianzisha umaarufu wake kote Afrika.

Mwaka wa 1992, bendi ilikabiliwa na msiba wake wa kwanza mkubwa wakati Emoro, mbilikimo wa kusakata rhumba wa bendi, aliupa dunia mkono wa buriani wakati walikuwa ziarani nchini Botswana. Licha ya msiba huu, umaarufu wa Pepe Kallé uliendelea kuenea katika miaka ya tisini kwani alitoa Albamu kama Gigantafrique, Larger than life na Cocktail . Alishirikiana na wanamuziki wa kitambo mashuhuri kama vilevile Lutumba Simaro na Nyoka Longo.
Pepe Kallé aliaga dunia kutokana na mshtuko wa moyo mnamo Novemba 1998.
No comments:
Post a Comment