Thursday, July 5, 2012

CORINTHIANS WATAWADHWA MABINGWA WAPYA AMERIKA KUSINI.


 

KLABU ya Corinthians ya Brazil imefanikiwa kunyakuwa kombe la Klabu Bingwa ya Amerika Kusini kwa jumla mabao 3-1 katika michezo miwili ya fainali waliyocheza dhidi ya klabu ya Boca Juniors ya Argentina. Wiki iliyopita Corinthians ilifanikiwa kutoa sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Boca ambapo katika mchezo wa marudiano klabu hiyo ya Brazil ilifanikiwa kubakisha kombe hilo nyumbani kwa kushinda mabao 2-0 katika uwanja wake wa Pacaembu. Mabao ya timu hiyo yalifungwa na mchezaji wao nyota Emerson katika dakika ya 36 na 73 ambapo sasa klabu hiyo itashiriki michuano ya kombe la Klabu Bingwa ya Dunia itakayofanyika Desemba mwaka huu nchini Japan. Ushindi huo umekata kiu ya mashabiki wa Corinthians ambao kwa miongo kadhaa imekuwa ni klabu pekee iliyopo katika jiji la Sao Paulo ambayo ilikuwa bado kunyakuwa taji hilo katika michuano mikubwa barani humo. Boca Juniors walikuwa wakitafuta taji hilo kwa mara ya saba ambapo ndio ingekuwa klabu pekee kunyakuwa taji hilo mara nyingi zaidi wakiwa pamoja na klabu ya independiente nayo ya Argentina.

No comments:

Post a Comment