Mtoto mmoja aitwaye Bonifance Edward mkazi wa kijiji cha Ilolo jijinj Mbeya amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye shimo la maji machafu wakati akicheza na watoto wenzake.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Bw.Diwani amesema tukio hilo limetokea julai 3 mwaka huu majira ya saa nane mchana katika eneo la Ilolo jijini hapa.
Diwani amesema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya.
Katika hatua nyingine Bw Athumani amewataka wazazi na walezi kuhakikisha mazingira yanayo wazunguka watoto na jamii kwa ujumla kuwa salama ili kuepukana na matatizo kama hayo.
No comments:
Post a Comment