SHIRIKISHO la Soka nchini Senegal limesema kuwa linajipanga kuingia katika kinyang’anyiro cha kutafuta nafasi ya kuwa mwenyeji wa michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2019 ikiwa ni miaka 20 toka nchi kutoka Magharibi mwa Afrika kuandaa michuano hiyo. Wizara ya michezo ya nchi hiyo imesema kuwa inaangalia uwezekano wa kuandaa michuano hiyo kwa pamoja na jirani zao Gambia ambao hawajawahi kuandaa michuano ya Mataifa ya Afrika. Mpaka sasa nchi hiyo haijatuma barua rasmi, hatahivyo waziri wa michezo wan chi hiyo El Hadj Malick Gackou aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanatarajiwa kutuma barua ya maombi kwa Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF mapema iwezekanavyo. Gackou aliendelea kusema kuwa mpango huo umekuwepo kwa kipindi kirefu sasa ambapo mji mojawapo ambao utatumika katika michuano ni wa Zinguinchor ambao ni wa pili wa ukubwa baada ya mji mkuu wa Dakar.
Wednesday, July 4, 2012
SENEGAL YAWANIA KUANDAA AFCON 2019.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment