Wednesday, July 4, 2012

GLOBAL NEWS: ARAFAT HUENDA ALIUAWA KWA SUMU

Mjane wa kiongozi wa zamani wa Paletstina, Suha Arafat, amesema mume wake alikufa kutona na sumu aina ya polonium.

Suha alitoa madai hayo wakati akihojiwa na kuĂ­tuo cha televisheni cha Al-Jazeera. Vipimo vya maabara nchini Uswisi vimeonyesha kuwepo kwa kemikali hiyo yenye kiwango cha juu cha miale katika vitu vya marehemu Yassar Arafat, jambo ambalo si la kawaida. Majane huyo  aliomba vipimo hivyo vifanyike na kukabidhi vitu binafsi vya marehemu mumewe zikiwemo chupi na misuwaki, kwa kituo cha Al-Jazeera, ambacho kilivituma kwa taasisi ya uchunguzi ilioyoko mjini Lausanne. Mjane huyo ametowa wito kwa mamlaka ya utawalawa ndani ya Palestina kuufukua mwili wa Arafat ili vipimo vingine vifanyike  katika uchunguzi wa kimataifa. Yassar Arafat alifariki katika hospitali ya kijeshi nje ya mji wa Paris Novemba 11, 2004 .Kwa miaka minane iliopita, ulizagaa uvumi miongoni mwa awapalestina kwamba kiongozi wao aliuawa.

No comments:

Post a Comment