Wednesday, July 4, 2012

MBEYA UPDATE: AFUMANIWA NA MUME WA MTU, AVUNJWA MGUU

Mkazi wa Mtaa wa Ilembo,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya Bi.Zainab Mapumba(40),ambaye ni mjane amejeruhiwa kwa kukatwa katwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake ukiwemo mguu wa kushoto uliovunjwa na kichwa kucharangwacharangwa.

Tukio hilo limetokea katika Mtaa wa Ilolo,ambapo inadaiwa kuwa mwanamke huyo mwenye watoto watano alikuwa na Bwana Juma Senka katika eneo la Grocery moja wilayani humo na mara baada ya kunywa pombe Bi. Mapumba alisindikiza Bwana Senka nyumbani kwake na walipofika upenuni mwa nyumba yake wote wawili walivua nguo na kuanza kufanya tendo la ndoa.

Mke wa Bwana Senka aliposikia kelele na kishindo alitoka nje akiwa na panga na kuwakuta watuhumiwa hao wakifanya mapenzi na kuamua kumwita mwanawe na kisha kuanza kumshambulia mjane huyo na kumjeruhi vibaya kichwani na pia kumvunja miguu.

Baada ya mkasa huo Bwana Senka alitoroka kusikojulikana kuepuka adha ya aibu na mkewe naye kutoroka kukwepa mkono wa sheria huku wasamaria wema wakimkimbiza Bi Mapumba katika Hospitali ya wilaya hiyo.

Aidha Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Nico Mbilinyi amesema kuwa mjane huyo alifikishwa hospitalini hapo Julai 2 mwaka huu majira ya usiku na kwamba hali yake inaendelea vema. 

Hata hivyo baadhi ya mashuhuda wamedai kuwa Mjane huyo alionywa mara kadhaa kuwa na kutokuwa na mahusiano na Bwana Senka,ambapo mkewe alikosa uvumilivu hivyo kupelekea kuanza kujichukulia sheria mkononi

No comments:

Post a Comment