Hivi karibuni mabondia Francis Cheka na Japhet Kaseba walitiliana mkataba na Promota wa ngumi za kulipwa Kaike Siraju katika pambano lisilo la ubingwa tarehe 7 July mwaka huu katika uwanja wa taifa jijini Dar-Es-Salaam.
Mkataba/mikataba hiyo iliidhinishwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC).
Baada ya makubaliano hayo bondia Francis Cheka alipewa fedha za awali (ambapo kinyume na taratibu za ngumi ambazo haziruhusu promota kutoa pesa kabla ya pambano kufanyika).
Hata hivyo tunashauri kuwa kama mmoja wa mabondia wahusika hatatokea katika pambano hili, sisi TPBC tunamruhusu promota wa pambano Kaike Siraju kumchukulia hatua za kisheria mkusika ikiwa ni pamoja na kumstaki mahakamani.
Kwa upande wa TPBC tutamfungia bondia yeyote ambaye atakiuka makubaliano aliyoingia na promota wa pambano.
Tutamfungia kucheza ngumi mahali popote duniani kwa kibali cha TPBC.
Tutafanya hivi kuKOMESHA mtindo ambao umeanza kutokeza wa mabondia kusaini mikataba na kuchukua malipo ya awali na baadaye kutishia kutocheza.
Huu ni utomvu mkubwa wa nidhamu na kauna tofauti yoyote ile na wizi wa pesa.
Imetumwa na:
Utawala
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC)
No comments:
Post a Comment