Tuesday, July 3, 2012

FREEMASONRY NAD JABIR JOHNSON: SEHEMU YA 17, TAFSIRI YA Abdullaah Bin Humayd KUHUSU UMASONI

SEHEMU YA 17
Azma ya mwanzo ya Umasoni ni kuupiga vita “Ukristo”. Baadaye, azma zao ziliendelea kupiga vita dini zote, kuirudisha tena Israel na kuitoa Palestine.


Malengo muhimu na imani zao kuu za wajumbe wa jumuiya hii ni:

1.                 Wanaitakidi kwamba imani kwa Allaah, Mitume na Vitabu kama ni upuuzi na hawaamini chochote katika ghayb.
2.                 Wanashiriki kwa hali zote kubadili serikali ili kuweka serikali ambayo inawakubali wao pamoja na mawazo yao.
3.                 Wanahubiri ukombozi wa ngono na kumuona mwanamke kama ni aina fulani ya umiliki.
4.                 Wanafanya bidii kuchana chana mataifa – isipokuwa taifa la Kiyahudi na kuanzisha migongano ya kudumu baina yao.
5.                 Wanauza na kutoa silaha kwa pande zote mbili ili kushinikiza mapigano.
6.                 Wanafanya kila jitihada ya kuendeleza ukabila na uadui.
7.                 Inaua na kuharibu kanuni za maadili kwa kutumia hongo kupitia ngono na pesa ili kuwavutia wenye kutoa maamuzi.
8.                 Wanafanya uchunguzi wa kudumu (na kuzifanyia kazi) ili kuwazuia Waislamu na kuwapunguza kupitia aina zote (birth control) na kongamano zinazoshajiisha mambo hayo kama vile: “Kongomano La Wazawa”.

Mwaka 1717 M, Umasoni ulijitokeza kwa jina jengine jipya: Jamii ya Kimasoni (Freemasonic Society) au Wamasoni (Freemasons), wakitekeleza malengo yake ya kupiga vita dini zote. Pia walichukua nembo mpya: Pembe tatu baadaye ikagaiwa (pande mbili), baadaye walianzisha kituo chao cha mwanzo cha Kimasoni nchini Uingereza, wakiwa na kauli mbiu mpya: uhuru, udugu na usawa. Baada ya hapo, walitoa maamuzi ya kuweka (wazi) maazimio yao ya kweli kama ifuatavyo:
1)    Kuuendeleza Uyahudi.
2)    Kupiga vita dini zote, haswa Ukatoliki.
3)    Kueneza ukafiri na ukombozi.

No comments:

Post a Comment