Thursday, July 5, 2012

MBEYA UPDATE: MGANGA WA TIBA ASILIA AUAWA MBOZI


Mganga mmoja wa tiba ya asilia  aliyefahamika kwa jina la Mwendapandi Mwafogo(78) ameuawa na watu wasiofahamika katika kijiji cha Sesanga Wilayani Mbozi  Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kishirikina.

Kamanda wa polisi mkoani mbeya Diwani Athumani amesema tukio hilo limetokea  mnamo july 3 mwaka huu majira ya saa nne za asubuhi katika kijiji cha Sesanga wilayani humo.

Athumani amesema kuwa mwili  wa marehemu ulikutwa umetupwa katika mto Harungu  ukiwa umenyogwa  na jeraha kubwa usoni, huku  mikono na miguu ikiwa imefungwa kwenye baiskeli yake.                                           

Hata hivyo Bw.Diwani amedai kuwa  marehemu anatuhumiwa kuwa  mchawi kwani alikuwa  anawasaidia wachawi kuloga watu kijijini hapo.

Aidha Bw.Diwani ameitaka jamii kuondokana na imani potofu za kishirikina  ikiwa ni pamoja  na kutojichukulia sheria mkononi.      

No comments:

Post a Comment