Wednesday, July 4, 2012

WENGER APANIA KUVUNJA BENKI KUMBAKISHA VAN PERSIE.

Robin van Persie.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ameitaka klabu hiyo kuvunja benki na kuhakikisha inambakisha mshambuliaji wao nyota Robin van Persie kabla ya msimu ujao wa Ligi Kuu nchini Uingereza haujaanza. Wenger alikaririwa akisema kuwa kwasasa wanahitaji kumbakisha mshambuliaji huyo kwa gharama yoyote kwasababu wanamtegemea kwa kiasi kikubwa. Kocha huyo ambaye anajulikana kwa ubahili tayari amebadilisha mfumo wa mishahara katika klabu hiyo ili kuhakikisha anamzuia nahodha wake huyo kwenda katika klabu ya Manchester City. Wenger aliendelea kusema kuwa amekuwa akimuunga mkono mchezaji huyo hata katika kipindi kigumu ambacho amepitia katika klabu hiyo hivyo sasa anaamini mchezaji huyo atamalizia soka lake kwenye klabu hiyo. Wenger ambaye amekataa ofa ya kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Laurent Blanc kujiuzulu, anaamini kuwa usajili wa paundi milioni 13 alioufanya kwa mshambuliaji wa klabu ya Montpellier Olivier Giroud utasaidia kumshawishi Van Persie kubakia.

No comments:

Post a Comment