Wednesday, July 4, 2012

GLOBAL NEWS: POLISI YAVAMIA NYUMBA YA SARKOZY

Polisi nchini Ufaransa wameivamia nyumbani na ofisini ya rais wa zamani wa nchi hiyo Nicolas Sarkosy.

Hatua hiyo ni katika uchunguzi wa madai kuwa rais huyo alifadhili kampeni zake mwaka 2007 kinyume na sheria. Uchunguzi huo unafuatia madai kuwa mwanamke tajiri zaidi nchini Ufaransa, ambaye ni mrithi wa kampuni ya vipodozi ya L'Oreal Cosmetics, Liliane Betterncourt - alitoa mchango katika kampeni hizo ambao haukuwekwa wazi. Sarkozy amekanusha kutenda makosa. Hii ni kesi ya kwanza inayomkabili Sarkozy, tangu aliposhindwa na msoshalisti Francois Hollande Juni 15 mwaka huu. Alikuwa akilindwa na kinga ya urais akiwa madarakani, ambayo ilizuwia asinfunguliwe mashtaka.

No comments:

Post a Comment