Monday, July 2, 2012

MTANANGE WA AL AHLY NA MAZEMBE KUPIGWA BILA YA MASHABIKI.

WIZARA ya Mambo ya Ndani nchini Misri imeamuru timu ya Al Ahly kucheza bila ya mashabiki katika mchezo wao wa Ligi ya Klabu Bingwa barani Afrika dhidi ya timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Al Ahly itakuwa mwenyeji wa Mazembe katika mchezo wa kwanza katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ambao utafanyika Julai 8 mwaka huu. Mkurugenzi wa Michezo wa Al Ahly, Mahmoud Alaam alithibisha klabu hiyo kupokea taarifa rasmi kutoka wizarani jana ikiwahitaji kucheza mchezo huo bila uwepo wa mashabiki wake. Wachezaji wengi wa Al Ahly walikuwa wakitegemea mashabiki wao kuwashangilia katika mchezo huo lakini hilo halitawezekana baada ya mameneja wa Uwanja wa Kijeshi ambao utatumika kwa ajili ya mchezo huo kukataa kwa sababu za kuisalama. Mwanzoni TP Mazembe waliliandikia barua Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF kutaka mchezo huo uchezwe nje ya nchi hiyo kwasababu za kiusalama.

No comments:

Post a Comment