Monday, July 2, 2012

INIESTA MCHEZAJI BORA EURO 2012.

KIUNGO wa kimataifa wa Hispania, Andres Iniesta ambaye ameisaidia timu yake hiyo kunyakuwa taji la pili mfululizo la michuano ya Ulaya iliyofanyika nchini Poland na Ukraine ametajwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo. Iniesta ambaye alitoa msaada mkubwa kwa timu yake ya Hispania katika nafasi ya katikati na kupelekea kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa ya kwanza kutetea taji lake kwenye michuano hiyo. Ofisa Mkuu wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Andy Roxburgh amesema kuwa kuna wachezaji wengi kama Andrea Pirlo wa Italia Xavi ambaye alishinda tuzo hiyo mwaka uliopita na Xabi Alonso walionyesha viwango vizuri katika michuano hiyo. Lakini Iniesta alionyesha uwezo wa hali ya juu zaidi ya wenzake hao kutokana na kuwa mbunifu, kasi na uwezo binafsi pale timu yake inapokuwa katika wakati mgumu. UEFA pia iliteua timu ya nyota wa Ulaya ambayo itaundwa na wachezaji kutoka nchi mbalimbali zilizoshiriki michuano hiyo ambao ni makipa: Gianluigi Buffon-Italia, Iker Casillas-Hispania, Manuel Neuer-Ujerumani, mabeki: Gerard Pique-Spain, Fabio Coentrao-Ureno, Philipp Lahm-Germany, Pepe-Ureno, Sergio Ramos-Hispania, Jordi Alba-Hispania. Wengine ni viungo Daniele De Rossi-Italia, Steven Gerrard-Uingereza, Xavi-Hispania, Andres Iniesta-Hispania, Sami Khedira-Ujerumani, Sergio Busquets-Hispania, Mesut Ozil-Ujerumani, Andrea Pirlo-Italia, Xabi Alonso-Hispania wakati washambuliaji ni Mario Balotelli-Italia, Cesc Fabregas-Hispania, Cristiano Ronaldo-Ureno, Zlatan Ibrahimovoic-Sweden, David Silva-Hispania.

No comments:

Post a Comment