Monday, July 2, 2012

BOLT ACHEMSHA TENA MBELE YA BLAKE.

MWANARIADHA nyota wa Jamaica Usain Bolt ameshindwa kutamba tena mbele ya mwanariadha mwenzake Yohan Blake baada ya kushika nafasi ya pili katika mbio za mita 200 ambazo ni mahsusi kwa ajili ya maandalizi ya michuano Olimpiki. Bolt ambaye anashikilia rekodi ya dunia kwa kukimbia kwa kasi zaidi, hiyo ni mara ya pili kushindwa mbele ya Blake ndani ya saa 48. Blake alimshinda Bolt katika mbio za mita 100 zilizofanyika Ijumaa na kufanya hivyo tena katika mbio za mita 200 ambazo alimaliza akitumia muda wa sekunde 19.80 wakitofautiana kwa sekunde 0.03. Akihojiwa mara baada ya mbio hizo Bolt amesema kuwa kushindwa kwake katika mbio hizo ni changamoto ya kuona wapi ambapo alikosea na kufanyia kazi eneo hilo tayari kwajili ya michuano ya Olimpiki itakayoanza kutimua vumbi Julai 27 mwaka huu jijini London, Uingereza. Naye kocha wa Bolt, Glen Mills amesema ana imani na mwanariadha wake huyo kwamba atarejea katika kiwango chake kutokana na uzoefu alionao kabla ya kuanza kwa michuano ya olimpiki.

No comments:

Post a Comment