Monday, July 2, 2012

MBEYA UPDATE: MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI AFUMANIWA NA MKE WA MTU

Mwimbaji maarufu wa Nyimbo za Injili Mkoani Mbeya(jina tunalihifadhi),ambaye pia ni mwalimu wa kwaya moja jijini Mbeya, amefumaniwa katika Mtaa wa Ilolo Kati akiwa na mke wa mtu majira ya saa 3 usiku.

Mwimbaji huyo ambaye pia hujihusisha na huduma kwa watoto yatima,amejikuta akinaswa na mume wa mwanamke huyo aliyekuwa naye na kuokolewa na wasamalia wema,ambapo mwimbaji huyo baada ya majadiliano ya masaa matatu alikubali kulipa fidia ya ugoni ya shilingi 500,000.

Aidha mwimbaji huyo amekiri kutenda kosa hilo na kuahidi leo kulipa shilingi 250,000 na kiasi kilichobaki akidai atamalizia Julai 8 mwaka huu.

Ameongeza kwa kuomba kuhifadhiwa kwa lengo la siri kutovuja na kudai kuwa atakuwa mwaminifu katika ulipaji wa deni na kuondoka baada ya kuacha maandishi na kuweka sahihi mbele ya mwenyekiti aliyejiuzulu hivi karibuni wa mtaa huo wa Ilolo Kati..

No comments:

Post a Comment