Thursday, June 21, 2012

ZIDANE AIONYA UFARANSA DHIDI YA INIESTA.

NYOTA wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane amewaonya wachezaji wa timu ya taifa ya nchi yake kuwa lazima wawe makini na kiungo mchezeshaji wa timu ya taifa ya Hispania, Andres Iniesta kama wanataka kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya Ulaya. Ufaransa ilipata kipigo cha kushangaza baada ya kufungwa mabao 2-0 na Sweden ambao walikuwa wameshaenguliwa katika michuano ya hiyo Jumanne na kusababisha timu hiyo ikimaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi D. Zidane ambaye amewahi kushinda taji la michuano hiyo akiwana Ufaransa mwaka 2000 anadhani kuwa Iniesta ambaye anakipiga katika klabu ya Barcelona anaweza kuwa mwiba mchungu katika mchezo baina ya timu hizo. Zinade ambaye ana umri wa miaka 39 aliendelea kusema kuwa kwa upande wake Iniesta ameonyesha kiwango cha hali ya katika kikosi cha Hispania katika michuano hiyo, hivyo asipochungwa vizuri anaweza kusababisha madhara yatakayopelekea Ufaransa kushindwa kufika nusu fainali ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment