Thursday, June 21, 2012

CONSTANT KUZIBA PENGO LA MUNTARI, MILAN.

KLABU ya AC Milan ya Italia imemsajili kwa mkpo kiungo Kevin Constant kutoka klabu ya Genoa kuziba nafasi ya Sulley Muntari ambaye atakuwa nje ya dimba kwa miezi mitano hadi sita baada ya kufanyiwa upasuaji jana. Muntari ameonyesha kiwango kizuri toka alipojiunga kwa mkopo na Milan Januari akitokea Inter Milan na alitarajiwa kusaini mkataba wa kudumu kabla ya kuumia mguu wakati wa mchezo wa kimataifa wa timu ya taifa ya Ghana. Taarifa kutoka klabu hiyo imesema upasuaji wa kiungo huyo umekuwa wa mafanikio na mchezaji huyo anaweza kurejea tena uwanjani baada ya miezi mitano au sita kama hakutakuwa na tatizo lingine litakalojitokeza. Kuumia kwa Muntari kumesababisha Milan kumchukua Constant mwenye umri wa miaka 25 kwa mkopo ambapo pia wanaweza kumchukua moja kwa moja na klabu yake ya Genoa ilithibitisha hilo.

No comments:

Post a Comment