Thursday, June 21, 2012

AFRICA NEWS: MAUAJI NIGERIA YAFIKIA 100


I
dadi ya watu waliouawa katika mapigano kaskazini mwa Nigeria imeongezeka na kufikia watu 100. 
Habari zinasema kuwa, mapigano makali yaliyojiri hapo jana huko kaskazini mashariki mwa Nigeria kati ya wanajeshi wa nchi hiyo na waasi, yamepelekea watu 100 kuuawa na wengine kujeruhiwa. Hata hivyo idadi rasmi ya uharibifu uliosababishwa na mapigano hayo bado haijatangazwa. Kabla ya hapo duru za habari kutoka hospitali nchini humo zilikuwa zimetangaza kuwa, watu wapatao 34 wameuawa katika mapigano hayo wakiwamo polisi watatu.
Mapigano kati ya vikosi vya jeshi la nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika na watu wenye silaha yameongezeka zaidi katika siku za hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment