Saturday, June 9, 2012

WORLD CUP 2014 QUALIFYING: TAIFA STARS DHIDI YA GAMBIA


T
IMU ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ leo inashuka katika dimba la Taifa jijini Dar es Salam kukwaana na Gambia ‘The Scorpions’ katika mchezo wa mchujo wa kuwania kucheza fainali za kombe la dunia 2014 zitakazopigwa nchini Brazil. 
Akizungumza na waandishi wa habari,kocha mkuu wa Stars,  Mdenmark Kim Poulsen  alisema kikosi kikosi chake kipo katika hali nzuri ya kimchezo ambao anaamini utakuwa na upinzani mkubwa.

 Hata hivyo, Poulsen alisikitishwa TFF kutompatia  DVD za mechi za Gambia ili iweze kuwasaidia katika maandalizi ya mchezo wa kesho na kuongeza kuwa hii ni mara ya pili kushindwa kupatiwa DVD hizo ambapo awali ilikuwa katika mchezo dhidi ya Ivory Coast ambapo Stars ililala mabao 2-0.

 Poulsen aliongeza kuwa wachezaji wake wapo katika hali nzuri isipokuwa Nurdin bakari, huku kiungo mshambuliaji Haruna Moshi ‘Boban’ aliyekuwa majeruhi hali yake ikiimarika na huenda leo akampanga dimbani.

 Hata hivyo mchezo wa leo  unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na hasa ikizingatiwa kila timu inahitaji ushindi ambapo Gambia ilitoka sare ya bao 1-1  Morocco na Morocco katika mchezo wao ulipigwa nyumbani wiki iliyopita. 

Kocha wa Gambia, Mtaliano Luciano Machini akizungumza jana katika mazoezi yao kwenye uwanja wa Karume, alisema  itakuwa ngumu kwa sababu wapinzani wao ni wazuri na wana kasi uwanjani.

 Mchezo huo utakapigwa kuanzia saa 10.00 jioni na kuchezeshwa na waamuzi kutoka nchini Zimbabwe,  Ruzive Ruzive akisaidiwa na Salani Ncube na Edger Rumeck.

No comments:

Post a Comment