Saturday, June 9, 2012

TANZANIA FOOTBALL STARS: NSAJIGWA KUJIUNGA NA GOR MAHIA YA KENYA


S
iku chache baada ya kutemwa na klabu yake ya Yanga, nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania Shedrack Nsajigwa sasa yupo nchini Kenya akifanya mazungumzo ya kujiunga na klabu kongwe ya nchi hiyo Gor Mahia.
Taarifa rasmi nilizozipata kutoka nchini Kenya zinasema kwamba Nsajigwa ametua Kenya juzi na jana amekutana na viongozi wa klabu ya Gor Mahia na so far mazungumzo yanaenda vizuri na muda wowote wanaweza kufikia makubaliano na Nsajigwa akajiunga na mtanzania mwenzie ambaye walikuwa wakicheza wote Yanga na timu ya Taifa, Ivo Mapunda.

No comments:

Post a Comment