Wednesday, June 27, 2012

WEMBLEDON DAY 2: NADAL, SERENA WASONGA MBELE.

MCHEZA tenisi anayeshika namba mbili katika orodha za ubora duniani, Rafel Nadal amefanikiwa kuanza vyema michuano ya Wimbledon baada ya kufanikiwa kumfunga Thomaz Bellucci katika mzunguko wa kwanza wa michuano hiyo. Nadal ambaye amewahi kushinda michuano hiyo mwaka 2008 na 2010 alifanikiwa kumfunga Bellucci wa Brazil 7-6 7-0 6-2 6-3 ambapo sasa anatarajiwa kukutana na Nicolas Almagro katika mzunguko wa pili wa michuano hiyo. Kwa upande wa wanawake mwanadada Serena Williams naye alianza vyema michuano hiyo baada ya kumfunga Barbora Zahlavova Strycova kwa 6-2 6-4 ambapo sasa atakutana na bingwa mtetezi wa michuano hiyo Petra Kvitova katika mzunguko wa pili wa michuano inayofanyika jijini London.

No comments:

Post a Comment