Wednesday, June 27, 2012

EURO 2012 NEWS: URENO Vs HISPANIA, KATIKA NUSU FAINALI YA KWANZA


L
EO ni kivumbi na jasho katika Nusu fainali ya Kwanza ya Michuano ya Mataifa ya Ulaya inayoendelea nchini Poland-Ukraine pale miamba ya Soka barani humo Ureno na Hispania itakapokutana katika uga wa Don Bass Arena  katika Jiji la Donetsk nchini Ukraine.

Wengi katika mechi hii wanaipa sana Hispania kuwa itasonga mbele licha ya kwamba mechi itakuwa ngumu itaanza kuchezwa majira ya saa 3:45 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, huku mwamuzi wa kati akiwa C. Cakir .

URENO
Timu ya taifa ya Ureno (Seleccao) inaingia uwanjani leo ikiwa na rekodi ya kuitandika Hispania (La Fuja Roja)  Novemba 2010 kwa mabao 4-0 katika Friendly Match miezi michache baadaye baada ya kuondolewa katika Michuano ya World Cup kwa bao 1-0. iliyochezwa katika Jiji la Lisbon.

Mechi 5 zilizopita
Jun 13, 2012 Denmark 2 - Portugal 3EC
Jun 9, 2012   Germany 1- Portugal 0EC
Jun 2, 2012   Portugal 1 - Turkey 3FR

Probable Lineup: Rui Patrício; Fábio Coentrão, Bruno Alves, Pepe, João Pereira; João Moutinho, Raul Meireles, Miguel Veloso; Cristiano Ronaldo, Luis Nani, Hugo Almeida.

HISPANIA
Ureno inaingia katika mechi ya leo baada ya kurusu bao moja tu katika mechi 8 za Knock out katika Euro/World Cup

Mechi 5 zilizopita
Jun 23, 2012 Spain 2 - France 0EC
Jun 18, 2012 Croatia 0 - Spain 1EC
Jun 10, 2012 Spain 1 - Italy 1EC
Jun 3, 2012   Spain 1 - China 0FR

Pia Xavi ndiye mchezaji pekee katika michuano hii kwa kupiga pasi nyingi kuliko wengine.

Probable Lineup: Iker Casillas; Jordi Alba,  Gerard Piqué, Sergio Ramos, Alvaro Arbeloa; Xabi Alonso, Sergio Busquets, Andrés Iniesta, Xavi Hernandez, David Silva; Cesc Fabregas

Mechi hii inajulikana kama “IBERIAN Game” kutokana na nchi hizo mbili kuwepo katika Pensula ya Iberian.

Pia kumekuwa na maswali mengi kama Andres Iniesta aataweza kweli kupenya katika ngome ya Seleccao hii leo.

No comments:

Post a Comment