Wednesday, June 27, 2012

BOCA, CORINTHIANS UWANJANI LEO KWENYE FAINALI YA COPA LIBERTADORES.

MABINGWA wa soka nchini Argentina klabu ya Boca Juniors wanajiandaa kutwaa taji la saba la kombe la Klabu Bingwa ya Amerika Kusini maarufu kama Copa Libertadores wakati watapokutana na klabu ya Corinthians ya Brazil katika fainali ya kwanza ya michuano hiyo itayotarajiwa kufanyika leo. Boca ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kunyakuwa taji hilo kutokana na rekodi ya kucheza fainali ya michuano hiyo mara nyingi zaidi ya wapinzani wao huku kiungo wake mchezeshaji mkongwe Juan Roman Riquelme akitegemewa kuonyesha cheche zake kwenye mchezo huo. Kocha wa Boca Julio Cesar Falcioni anatarajiwa kutumia kikosi kilekile ambacho kiliiondosha timu ya Universidad ya Chile katika hatua ya nusu fainali. Finali hiyo ya kwanza inatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa La Bombonera ambao ni uwanja wa nyumbani wa Boca uliopo katika jiji la Buenos Aires nchini Argentina. Corinthians itacheza fainali ya michuano hyo kwa mara ya kwanza baada ya kufanikiwa kuifunga Santos kwa jumla ya mabao 2-1 katika michezo miwili waliyokutana lakini ugeni wao katika michuano hauwezi kuwazuia kuifunga Boca haswa kutokana na kiwango cha hali ya juu ambacho wamekionyesha safari hii.

No comments:

Post a Comment