Sunday, June 17, 2012

URUSI ILISTAHILI KUTOLEWA - VERHEIJEN.

KOCHA wa viungo wa timu ya taifa ya Urusi, Raymond Verheijen anaamini kuwa kikosi chake hicho kilistahili kutolewa katika michuano ya Ulaya baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Ugiriki katika mchezo wa kundi A uliochezwa jana. Verheijen mwenye umri wa miaka 40 aliteuliwa kuwa kocha wa viungo wan chi hiyo na kocha wa kikosi hicho Dick Advocaat ambaye wote wanatoka Uholanzi baada ya kufanya kazi kama kocha msaidizi katika timu ya taifa ya Wales mpaka Februari mwaka huu. Dakika chache baada ya Urusi kuondolewa katika michuano hiyo na Ugiriki katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Warsaw alituma ujumbe katika mtandao wa kijamii wa Twitter akizipongeza timu ambazo zilisonga mbele katika michuano hiyo. Kocha huyo amesema kuwa Urusi walistahili kutolewa kwani walimiliki mchezo kwa asilimia 80 katika kipindi chote cha pili lakini kulikuwa hakuna ubunifu hivyo kushindwa kutengeneza nafasi za kufunga. Urusi ilitolewa katika michuano hiyo baada ya kushika nafasi ya tatu katika kundi A wakiwa wamjikusanyia alama nne katika michezo mitatu waliyocheza.

No comments:

Post a Comment